Burudani
Gwajima: Mungu ameweka kitu kwa Dudubaya, aache matusi
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amesema msanii Dudubaya ana kitu ambacho amepewa na Mungu na endapo ataacha matusi kitu hicho kitaza faida kubwa.

Dkt. Gwajima ametoa kauli hiyo wakati akihojiwa kuhusu kauli ya Dudubaya ambayo anapenda kuitumia ya 'you better watch your back' akimaanisha linda mgongo wako.
Waziri huyo amesema ni jambo zuri kwa msanii huyo kufanya kampeni ya kupinga ushoga na usagaji.
Hata hivyo, Dkt. Gwajima amemtaka Dudubaya kutumia lugha nzuri na yenye kujenga katika kufikisha ujumbe wake, akieleza kuwa anaweza hata kupewa nafasi ya kuwa balozi wa kampeni hiyo.
“Hakuna mtu aliyekamilika duniani, Dudubaya akiacha matusi ana kitu kikubwa ambacho Mungu kamjalia,” amesema Gwajima.
- Dorothy Gwajima
- Dudubaya
- Muziki