Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Burudani

Usher aonyesha sebule ya jumba lake

MWANAMUZIKI na nguli wa R&B, Usher Raymond ameonyesha muonekano wa kipekee wa sebule ya jumba lake la kifahari lililopo Atlanta, Georgia, Marekani kupitia jarida mashuhuri la Architectural Digest.

Jumatatu, 10 Agosti 2026 · 17:15Dakika 1 kusomaToleo 177, uk. 40

Sebule ya jumba hilo, imetawaliwa na sofa ya kipekee ya plasiki yenye mikunjo iliyobuniwa kwa ushirikiano kati ya Usher na mbunifu wa muonekano wa ndani, Nicole Fuller.

Juu ya sofa hiyo kuna mchoro mkubwa wenye rangi za kuvutia uliochorwa na msanii mashuhuri duniani, Damien Hirst.

Katikati ya sofa hizo kuna meza yenye muundo wa kiumbe wa kiasili (sanamu), iliyochongwa na wabunifu maarufu duniani, Campana Brothers.

  • Usher
  • Muziki
  • Marekani

Soma Pia