Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Habari

HERO yawekeza ulinzi, usalama wa mtoto

MALEZI bora katika makuzi ya mtoto ni msingi wenye afya, mafanikio na ustawi kwa jamii inayojitambua.

Jumatatu, 17 Agosti 2026 · 17:15Dakika 2 kusomaToleo 178, uk. 28

Hakika ni kwamba mtoto anayelelewa kwa upendo, nidhamu na maadili hukua akiwa na tabia njema, hekima na mwenye kujitegemea kifikra mapema.

Kupitia malezi hayo, jamii hupanda mbegu za uaminifu, bidii na huruma ambazo baadaye humfanya mtoto awe raia na ama kiongozi mwema.

Mtoto anayelelewa vizuri leo ndiye atakayejenga taifa bora la kesho.

Kwa kutambua hilo, Taasisi ya Health and Education at Risk Organization (HERO), imeanza kuhamasisha jamii na hasa wazazi, kuwajibika katika malezi sahihi ya watoto, ikiwa na lengo la kupunguza Mtendaji Mkuu wa HERO, Joseph Kayinga HERO yawekeza ulinzi, usalama wa mtoto wimbi la watoto wanaojilea wenyewe na wanaofanya kazi mitaani.

Mtendaji Mkuu wa HERO, Joseph Kayinga, anasema lengo jingine la kampeni hiyo ni kupambana na umaskini wa kipato, fikra hasi na maisha bwete.

“Shauku yetu ni kuongeza tija ya watu wetu kwa kutumia taaluma ya ustawi wa jamii uzalishaji mali na kipato, kupitia kilimo, biashara na ufugaji,” anasema.

Katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, asasi hiyo imekuwa ikishughulikia mashauri matatu katika kata za Mabibo, Mbweni Mabwepande na Bunju jijini Dar es Salaam.

Mashauri hayo yanalenga kuimarisha usalama wa mtoto na kuhakikisha anapata ulinzi unaostahiri na malezi bora kutoka kwa wazazi wote wawili.

“Katika kuhakikisha kila mtoto anapata malezi yanayofaa, hata watoto wanaokutwa na changamoto ya kubaki kwenye familia, serikali inaagiza kwamba mtoto huyo atasaidiwa kwa kupelekwa kwenye makao ya kulea watoto wenye changamoto baada ya juhudi nyingine zote za kuhudumiwa akiwa kwenye familia ya asili kushindikana,” amesema Kayinga.

Sambamba na hilo, anasema asasi yake imepanua ushirikiano wa kimataifa kwa kutekeleza miradi miwili ya kimkakati ya kimataifa itakayohusisha nchi tano; mbili zikiwa Afrika na zinazosalia nje ya Afrika.

“Mradi mkuu unajulikana kama, International Social Workers Exchange Partnership (ISWEP) ambao ulianza mwaka 2018 kwa kushirikiana na wataalamu wa Ustawi wa Jamii wa Jiji la Hamburg, Ujerumani.

Anaongeza kuwa mpango huo umekuwa ukilenga ubadilishanaji wa maarifa baina ya wataalamu wa ustawi wa jamii.

Anaeleza kuwa tangu kuanza kwa mpango huo mwaka 2018, wataalamu wa ustawi walioshiriki walinufaika kwa viwango tofauti, lakini pia taasisi na vituo vilivyohusishwa vilipata uzoefu kila kimoja kwa namna yake.

Anataja changamoto kadhaa zilizojitokeza na pia kulikuwa ukiukwaji wa maadili nje ya utaratibu uliowekwa kiasi cha kusababisha asasi yake kukemea wahusika na hata kuchukua hatua za haraka pamoja na uchunguzi wa kina.

Kati ya hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kubadilisha utaratibu kwa kutunga sera na miongozo mipya ya usimamizi na uteuzi wa washiriki.

  • Watoto
  • Malezi
  • HERO

Soma Pia