Uhusiano
Mtoto anahitaji muda wa mzazi
HABARI za leo msomaji wangu wa Safu ya Uhusiano karibu tuungane pamoja kujulishana masuala mbalimbali ya maisha.

Kwa siku zilizopita nimepokea ujumbe kutoka kwa wasomaji na baadhi ya maoni yakieleza baadhi ya wazazi kushindwa kutenga muda wa kukaa pamoja na watoto wao kwa mazungumzo na masuala yatokanayo na masomo na mambo mengine.
Amina Jumanne wa Dar es Salaam anasema “Baba wa watoto wangu anafanya kazi kwa saa 12, anarudi nyumbani, anakula, analala, wiki nzima hajui watoto wake wameishije nyumbani na shuleni; Pesa ipo, lakini upendo na ushauri h a u p o.”
Joseph Lambart, mkazi wa Arusha anasema enzi za ujana wake akiwa na wazazi aliishi nao na kupewa kila kitu, lakini wazaza hawakuwa na muda wa kukaa naye na kumuuliza changamoto na mengine mazuri na matokeo yake alitafuta upendo nje.
Mama Neema Jackson wa Mwanza anasema tatizo siyo kukosa muda, bali ni vipaumbele.
“Unakuta mzazi ana muda wa kuperuzi Mtoto anahitaji muda wa mzazi Na Anti MSHAURI mitandaoni kama Tik Tok pengine kwa saa nzima, lakini anakosa dakika 10 za kukaa na mtoto wake na kusikia mazuri yake na changamoto anazopitia.
Maoni ya wasomaji hawa yanatafakarisha mengi. Suluhisho la haya yote ni kutenga muda maalum na watoto; chagua dakika 20 walau mara mbili au tatu kwa wiki. Hakuna simu, hakuna Televisheni, jitahidi kuuliza tu, leo(siku husika) kulikuwaje? Na na umsikilize vyema.
Lakini pia shiriki majukumu; baba na mama siyo kazi ya mtu mmoja; mmoja anafundisha hesabu, mwingine anasoma Biblia au hadithi na jingine jitahidini kuwa mfano kwa watoto.
Mtoto anajifunza kwa kukutazama kama wewe unakuwa umeshika simu wiki nzima na kuacha kuwa nao pamoja unamjenga kuiga ufanyayo.
Wazazi eleweni kuwa pesa italisha mtoto leo lakini muda wako ndio utamlea awe mtu wa kesho.
Tukutane wiki ijayo.
- Malezi
- Familia
- Ushauri