Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Michezo

Huyo Raphinha nyie msikieni tu!

MSHAMBULIAJI wa pembeni wa Timu ya Barcelona ya Hispania, Raphael Dias Belloli ‘Raphinha’ ameendeleza moto wa kufumania nyavu za wapinzani kwa kupachika mabao 12 katika michezo saba ya ligi kuu ya nchi hiyo, La Liga -2026/27.

Jumatatu, 21 Septemba 2026 · 06:00Dakika 1 kusomaToleo 183, uk. 38

Katika mchezo wa Barcelona dhidi ya Sevilla uliochezwa mwishoni mwa wiki – Jumamosi, Septemba 19, Raphinha aliiwezesha timu yake kurejea mchezoni baada ya kuwa nyuma kwa bao 1 dhidi. Alifunga mabao yote matatu kwa timu yake.

Raphinha alichomoa na kuongeza kamba nyigine mbili na kupiga hattrick ambayo ni ya pili msimu huu katika michezo saba. Aliweka kimiani mabao matatu dhidi ya Racing; kuifunga Valancia bao moja; kufunga mabao mawili dhidi ya Vallecano; mabao mawili dhidi ya Eche huku akifunga moja dhidi ya Bilbao.

  • Raphinha
  • Barcelona
  • La Liga
  • Soka

Soma Pia