Michezo
Wazee wa kazi chafu EPL
KLABU za Brentford, Brighton na Bournemouth zimekuwa tishio kwa namna zinavyotembeza vipigo kwa vigogo wa Ligi Kuu ya England ‘EPL’ msimu huu 2026/27.
Mwishoni mwa wiki dunia iliwashuhudia mabingwa watetezi Arsenal wakichezea chuma tatu bila majibu kutoka kwa Brighton, Chelsea wakalambishwa sakafu na Brentford kwa mabao 3 -0.
BBB siyo umoja wa kuwashughulikia vigogo pale EPL pekee, bali ni klabu zilizojengwa kwenye misingi ya klabu haswa, wachezaji wake wengi wanauzwa na klabu inabaki na mifumo ambayo inaziwezesha kuleta nyota wapya na kuwatumbukiza kwenye vikosi vyao na kiwango cha michezo yao inabaki kuwa kama awali.
Ubishi wa klabu hizo unatokana na kukosa hofu, hazina cha kupoteza dhidi ya vigongo, bali vigogo ndio wenye presha ya ubingwa, mashabiki na ustawi wa klabu zao.
Je, nini kitarajiwe kwenye michezo mingine ijayo kwa timu hizo maarufu kwa jina la BBB? Tusubiri.
- EPL
- Brentford
- Brighton
- Bournemouth
- Soka