Michezo
Yamal mshindani wa hofu yake
NYOTA wa klabu ya FC Barcelona na Timu ya Taifa ya Hispania, Lamine Yamal, ameonyesha shaka yake juu ya imani ya familia yake kwake, siku atakayokosa ushindi vitani.
Amesema kuwa msamiati wa kushindwa kwa familia yake umekuwa mgumu, ingawa amekuwa akiwakumbusha kwamba mchezo wa mpira una matokeo matatu; kufunga, kufungwa ama kutoka sare.
Yamal ambaye kwa sasa ni miongoni mwa wachezaji wanaong’ara na kutajwa kuwa mchezaji bora duniani, alionyesha shaka hiyo wakati wa mahojiano na Gazeti la ‘The Guardian’ mwishoni mwa juma lililopita.
Shaka ya Yamal kwa familia yake, inaonyesha wazi kuwa kitu pekee ndugu zake wanajua na wanakiishi ni kwamba kijana wao ndiye nyota mwenye kipaji kikubwa kwa sasa ulimwengu wa soka, hivyo anapaswa kuleta furaha nyumbani katika kila mchezo na mashindano anayowakilisha klabu yake na taifa lake.
“Tatizo ni kwamba familia yangu haijui kuwa ni vigezo gani vya kushindwa, wao wanajua ushindi kwa kila mchezo ninaoshiriki…”.
“Baada ya Fainali za Kombe la Dunia, familia yangu ilikuwa na furaha sana, inaonekana kama jambo rahisi sana, wakati fulani nilijiambia siku ambayo sitashinda, je, watafikiri mimi sifai.?
Alijihoji Yamal.
Kutokana na kauli hiyo, ni wazi mshindi huyo wa Kombe la Dunia, sasa anaishi kwa kujituma zaidi ili kuweka familia yake kwenye furaha kila mara.
Umebakiwa na makala 2 za bure mwezi huu. Jiunge ili kusoma bila kikomo.
- Yamal
- Barcelona
- La Liga
- Soka