Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Jukwaa la CEOs kuwa chachu ya utekelezaji wa Dira 2050

Serikali inataka Mashirika ya Umma kuongeza tija na ufanisi ili uwekezaji mkubwa unaosimamiwa na taasisi hizo utoe matokeo yanayoonekana katika uchumi na kuwa nguzo muhimu ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Jumamosi, 26 Septemba 2026 · 16:08Dakika 3 kusoma
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Makalla (Katikati), akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Mkutano wa Watendaji wakuu wa taasisi za serikali ulioandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR). Ameambatana na Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiani wa OTR, Sabato Kosuri.

Serikali imesema Mkutano wa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma (C-CEOs Forum) 2026, unaotarajiwa kuwakutanisha viongozi kutoka Mashirika zaidi ya 300 ya Umma, pamoja na wawakilishi wa Sekta Binafsi na washiriki wengine zaidi ya 700 kuanzia Septemba 28 hadi 30, 2026, utakuwa jukwaa muhimu la kuimarisha utendaji, tija na mchango wa Mashirika hayo katika utekelezaji wa Dira 2050.

Mkutano huo, unayoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR), ni ya nne kufanyika tangu kuanzishwa kwake mwaka 2023 na inalenga kuwakutanisha Wenyeviti wa Bodi, Watendaji Wakuu wa Mashirika ya Umma na wadau mbalimbali kujadili namna ya kuongeza ufanisi wa taasisi hizo na kuhakikisha mipango na shughuli zao zinaendana na vipaumbele vya kitaifa vilivyoainishwa katika Dira 2050.

Kikomo cha bure kimefikia

Umesoma makala 3 za bure mwezi huu

Jiunge ili kuendelea kusoma bila kikomo, au ingia kama tayari una uanachama.

Mwezi

TSh 8,000

kwa mwezi

Mwaka

TSh 80,000

kwa mwaka

Au fungua akaunti ya bure ili hesabu yako ifuatane nawe kwenye vifaa vyote.

Lipa kwa M-Pesa · Mixx by Yas · Airtel Money · HaloPesa

Soma Pia