Burudani
Kajala adai milioni 200 kwa Mwijaku
Kajala ataka amtaka Mwijaku kumlipwa Shilingi milioni 200 kwa madai ya kumchafulia jina lake kwa umma kupitia mitandao ya kijamii.

MWIGIZAJI wa filamu, Kajala Frida Masanja kupitia mawakili wake, amemtaka Burton Mwemba maarufu Mwijaku kuacha mara moja kutoa, kuchapisha au kusambaza kauli anazodai zinamdhalilisha na kumchafulia jina.
Katika barua ya kisheria iliyotumwa kwa Mwijaku, mawakili hao wamedai kuwa video na kauli zake zinazomhusu Kajala zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii na zinaweza kuharibu heshima, sifa na maslahi yake ya kibiashara.
Mawakili hao wamemtaka Mwijaku aondoe video, machapisho na maudhui yote yanayolalamikiwa, pamoja na kutoa ahadi kwa maandishi ndani ya saa 48 kwamba hatarudia kufanya hivyo.
Aidha, Kajala kupitia mawakili wake amemtaka Mwijaku kulipa Shilingi milioni 200 ndani ya siku 14 kama fidia kwa madai ya madhara ya sifa, msongo wa kihisia, madhara ya kijamii pamoja na hasara za kiuchumi na kibiashara baada ya kusambazwa kwa video hizo na Mwijaku.
- kajala
- mwijaku
- fidia
- kuchafuliwa