Afya ya Kimwili
Kwa nini kiharusi hutokea zaidi asubuhi?
SAA za asubuhi hubeba hatari ya kiafya ambayo watu wengi hawaijui.
Utafiti wa kisayansi hivi karibuni umethibitisha kuwa kiharusi (stroke) hufuata mzunguko wa kibaolojia wa mwili, huku kiwango cha juu zaidi cha matukio haya kikitokea asubuhi na mapema, yaani kati ya saa 12 na saa 3 asubuhi.
Katika kipindi hiki, mtu anakuwa kwenye hatari zaidi - asilimia 40 hadi 55, ya hupata kiharusi kutokana na damu kutofika kwenye ubongo (ischemic stroke), au kwa sababu ya kupasuka kwa mishipa ya damu na damu kivilia kwenye ubongo (hemorrhagic stroke), au shambulio la muda mfupi la kiharusi (TIA) ikilinganishwa na muda mwingine wowote wa siku.
Mabadiliko ya kibaolojia “morning surge”.
hutokea pale mwili unapojiandaa kutoka kwenye usingizi na kuamka. Ili kukuandaa kwa ajili ya siku, ubongo hutoa kwa kasi homoni za msongo wa mawazo (cortisol na adrenaline).
Uzalishwaji huu wa homoni husababisha kupanda kwa haraka kwa shinikizo la damu na mpigo wa moyo.
Wakati huohuo, baada ya kulala kwa saa saba hadi nane bila kunywa kimiminika chochote, mwili huamka ukiwa na upungufu wa maji, jambo linalofanya damu kuwa nzito.
Seli za kugandisha damu (platelets) nazo huwa na mwelekeo wa kibaolojia wa kushikana zaidi masaa ya asubuhi na kutengeneza mazingira rahisi ya damu kuganda na kuziba mishipa.
Kwa wazee au watu wenye shinikizo la juu la damu, kuta za mishipa ya damu hushindwa kuhimili mabadiliko haya ya ghafla.
Mara kadhaa kumekuwa na maswali ambayo yanakosa majibu na hali hii inachochea kuhusianisha na imani za kishirikina.
Katika makala yetu wiki hii tutaangalia sababu mbalimbali kulingana na tafiti zilizofanyika ambazo zinajibu maswali mengi yaliyoko kwenye jamii yetu.
Mbali na mengi yanayotokea, msongo wa mawazo (stress) unazidisha zaidi hatari hii ya asubuhi. Ni kweli tafiti mbalimbali zinaonyesha jinsi msongo wa mawazo wa muda mfupi na wa.
- Kiharusi
- Afya
- Asubuhi
- Shinikizo la Damu