Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Burudani

Lionel Richie ‘awaponda’ Usher, Chris Brown

MWANAMUZIKI mkongwe kutoka Marekani, Lionel Richie amewakosoa Usher Raymond na Chris Brown kuhusu ziara yao ya pamoja, akisema wasanii wawili wakubwa kushirikiana kwenye ziara siyo jambo jipya.

Jumatatu, 17 Agosti 2026 · 17:15Dakika 1 kusomaToleo 178, uk. 38
Lionel Richie, Chris Brown
Lionel Richie, Chris Brown — Picha na Yahoo

Mkongwe huyo akiwa jukwaani katika ziara yake na kundi la Earth, Wind& - Fire, amesema wasanii hao wanaonekana kama wanajaribu kufanya jambo jipya, lakini yeye na wenzake walikuwa wakifanya aina ya ziara takriban miaka 40 iliyopita.

Richie akatoa utani uliowafanya mashabiki kucheka na kushangilia, akisema tofauti kubwa kati ya kizazi chao na cha Usher na Chris Brown ni kwamba wao “hawakwenda jela.”

Kauli hiyo ilionekana kulenga hasa historia ya matatizo ya kisheria ya Chris Brown.

Chris Brown amewahi kukabiliwa na kesi mbalimbali za kisheria, ikiwemo kesi maarufu ya mwaka 2009 iliyohusisha shambulio dhidi ya Rihanna.

Kwa hiyo, utani wa Richie ulitafsiriwa na wengi kama dongo la moja kwa moja kwa Brown, ingawa jina la Usher pia lilitajwa katika kauli hiyo.

  • Lionel Richie
  • Usher
  • Chris Brown

Soma Pia