Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Habari

Mawakili kupambana kesi ya Lissu

Katika uamuzi wa Ijumaa iliyopita, jopo la majaji watatu wanaosikiliza kesi hiyo wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, liliamua Lissu ana kesi ya kujibu katika kesi hiyo ya uhaini inayomkabili, hatua inayofungua njia kwa mwa- “Kwa hiyo hakuna haja ya kuwaita mashahidi hao ambao kwa kuwa ushahidi wao umeshatolewa na watumishi wa serikali, ni kama vile anataka hawa wafike ili afanye cross examination (awafanyie mahojiano) ya kile kilichoelezwa na mashahidi hao,” alisema.

Jumatatu, 24 Agosti 2026 · 06:00Dakika 3 kusomaToleo 179, uk. 12
Mawakili wa serikali wakiwa Mahakama Kuu kwenye Kesi ya Lissu
Mawakili wa serikali wakiwa Mahakama Kuu kwenye Kesi ya Lissu — Na Mpigapicha Wetu

Pia alisema hoja yake inasimama katika msingi mkuu wa kifungu cha nane cha Sheria ya Ulinzi wa Rais (Presidential Affairs Act) kinachoainisha kinga mbili kuu za kisheria kwa mkuu wa nchi.

Kinga hizo ni dhidi ya kukamatwa kwamba rais aliyeko madarakani hawezi kukamatwa wala kuzuiliwa chini ya sheria yoyote na kinga ya kutofika mahakamani, kwamba hakuna amri ya mahakama au wito wa kisheria unaoweza kumlazimisha Rais kufika mahakamani kibinafsi wakati anatumikia muhula wake.

Hoja hizo zilipingwa vikali na Lissu ambaye alisema tuhuma dhidi yake zinamhusu moja kwa moja rais ambaye ndiye mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama pamoja na wasaidizi wake, makamu na waziri mkuu ambao wote ni wajumbe wa baraza hilo.

Alisema tuhuma za uhaini ni nzito na zinazohusu tishio la usalama kwa taifa, hivyo mwenyekiti wa baraza la usalama la taifa ni lazima awepo ili kuthibitisha uwepo wa tishio hilo.

Lissu alieleza kuwa iwapo kuna hoja kwamba rais hawezi kufikishiwa wito moja kwa moja, utaratibu unaeleza wazi kuwa anaweza kufikishiwa wito huo kupitia kwa katibu mkuu kiongozi au kupitia kwa katibu wake binafsi, bila kujali kama ataupuuza au laa.

Mvutano baina ya pande hizo mbili unatarajiwa kuendelea katika utetezi wa Lissu unaotarajiwa kuendelea leo, wakati kesi hiyo itakapoendelea kusikilizwa.

Katika kesi hiyo, Lissu alikamatwa Aprili 9, 2025 muda mfupi baada ya kuhutubia mkutano wa chama chake, Chadema mjini Mbinga, kusini mwa Tanzania, ambapo siku iliyofuata, Aprili 10, 2025, alifikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Alishtakiwa kwa kosa la uhaini, pamoja na shtaka jingine la kuchapisha taarifa zinazodaiwa kuwa za uongo. Shtaka la uhaini ni miongoni mwa makosa mazito zaidi katika sheria za Tanzania.

Upande wa mashtaka uliwasilisha mashahidi 17 ambao baada ya kumaliza kuwasilisha ushahidi wake, mahakama ilitoa uamuzi kwamba ushahidi huo unatosha kumtaka Lissu ajitetee, kwa kuwa amekutwa na “kesi ya kujibu”.

“Mahakama imeamua kwamba upande wa mashtaka umejenga kesi ambayo mshtakiwa anapaswa kuijibu,” alileza Jaji Ndunguru wakati akitoa uamuzi huo Ijumaa iliyopita.

Jaji Ndunguru alieleza kuwa mahakama ilifikia uamuzi huo baada ya kuchunguza ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka pamoja na hoja za Lissu, ambaye aliiomba iachilie mbali kesi hiyo kwa madai kwamba hakuna ushahidi wa msingi unaomhusisha na kosa la uhaini.

Makamu Mwenyekiti wa Chadema, John Heche (kushoto), akiwa na Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani, Boniface Jacob wakati wa kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu katika Mahakama Kuu, Masjala ndogo ya Dar es Salaam juzi.

(Picha na Pambazuko).

Jaji Ndunguru alisema jukumu la mahakama katika hatua hiyo lilikuwa kuamua ikiwa ushahidi wa upande wa mashtaka, endapo hautapingwa, unaweza kutosha kumtia mshtakiwa hatiani.

Alisema mahakama haikuhitajika kufanya uchambuzi wa kina kuhusu uzito au uaminifu wa kila ushahidi katika hatua hiyo na masuala hayo yatazingatiwa baada ya Lissu kuwasilisha utetezi wake.

Kwa mujibu wa mahakama, ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka ulimhusisha Lissu kwa kiwango kinachotosha na matamshi yaliyowekwa katika hati ya shtaka.

Upande wa mashtaka uliita mashahidi 17 Stendi mpya ya daladala inayojengwa eneo la Mbezi, Dar es Salaam ambayo ilikuwa iwe mbadala wa stendi ya zamani, sasa imegeuzwa maegesho ya maroli kama ilivyokutwa na kamera ya Pambazuko jana.

ya kufunga ushahidi wake Agosti 17, ambapo waendesha mashtaka waliiambia mahakama kwamba ushahidi huo ulitosha kuthibitisha hoja muhimu za shtaka na kumtaka Lissu ajitetee.

Lissu anakabiliwa na shtaka moja la uhaini chini ya Kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu ya Tanzania, kutokana na matamshi anayodaiwa kutoa Aprili 3, 2025, katika mkutano uliofanyika katika makao makuu ya Chadema jijini Dar es Salaam.

Upande wa mashtaka unadai kwamba matamshi hayo yalihusiana na msimamo wa Chadema wa kutoshiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 bila kufanyika kwa mageuzi ya mfumo wa uchaguzi.

Waendesha mashtaka wanadai kwamba Lissu alihamasisha wananchi kuzuia uchaguzi huo na kutoa matamshi yaliyokusudiwa kuishinikiza na kuitishia serikali.

  • Tundu Lissu
  • Mahakama
  • Chadema

Soma Pia