Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Habari Kuu

Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar yaiva

Sasa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK) iko tayari. Bado hatua chache tu - pengine ya kutangazwa rasmi, kwani mambo mengi yamekamilishwa.

Alhamisi, 17 Septemba 2026 · 10:52Dakika 2 kusomaToleo 182, uk. 28
Rais Mwinyi na Othman Masoud Othman.
Rais Mwinyi na Othman Masoud Othman. — Picha kutoka Maktaba ya Pambazuko

RAIS wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameitangaza Kamati ya Pamoja ya Majadiliano itakayofuatilia na kuchambua mambo yaliyokubaliwa na vyama viwili vya siasa vilivyokamilisha mazungumzo ya kuondoa mvutano wa kisiasa ulioibuka tena baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana.

Kamati hiyo itaongozwa na wenyeviti wawili, mmoja kila upande kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha ACT Wazalendo.

Taarifa ya Ikulu ya Zanzibar, iliyotolewa jana na Katibu wa Baraza la Mapinduzi (BLM) na Katibu Mkuu Kiongozi, Mansura Mossi Kassim, Rais amemteua Abdi Mahmoud Abdi kutoka CCM na Omar Ali Shehe kutoka ACT Wazalendo kuiongoza kamati itakayokuwa na wajumbe kumi.

Wateuliwa hao wawili ambao wote kwa sasa ni manaibu katibu wakuu wa vyama vyao upande wa Zanzibar, wanakuwa wajumbe na wakati huohuo wenyeviti wenza wa kamati hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi leo katika hafla itakayofanyika Othman Masoud Othman Ikulu mjini hapa majira ya Saa 5 asubuhi.

Wajumbe wengine wanaounda kamati hiyo ni Dkt. Khalid Salum Mohamed, Najma Murtaza Giga, Masoud Ali Mohamed na Mgeni Hassan Juma wanaotoka CCM.

Dkt. Khalid ni Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi anayewakilisha jimbo la uchaguzi la Donge, Wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja, na pia Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi kwenye serikali iliopo ambayo Dkt. Mwinyi aliiunda baada ya uchaguzi huo wa Oktoba 2025.

Masoud naye ni Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa kuteuliwa na rais. Mgeni ni Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia Viti Maalum wanawake, na ameendelea kuwa Naibu Spika katika Baraza la Wawakilishi kwa kipindi cha tatu mfululizo sasa.

Giga naye ni Mbunge wa Viti Maalum akiwa pia mmoja wa wenyeviti wanaomsaidia Spika na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuongoza vikao.

Wajumbe wanne wengine kutoka ACT Wazalendo ni Omar Said Shaaban, Fatma Abdulhabib Fereji, Said Ali Mbarouk na Mohamed Nur Mohamed. Omar ambaye kitaaluma ni mwanasheria na wakili nchini, ndiye Mwanasheria Mkuu wa ACT wakati Fereji, mwalimu kitaaluma, kwenye chama ni Katibu wa Ngome ya Wanawake.

Aidha, wote Omar na Fereji, pamoja na Mbarouk, waliwahi kuwa mawaziri katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

Taarifa ya Ikulu pia imetaja kuwepo kwa makatibu wa kamati ambako walioteuliwa ni Mwalim Ali Mwalimu Seif Khamis Mohamed. Na imeundwa sekretatieti ya kamati ambayo taarifa inawataja wajumbe wake kuwa ni Hamid Saleh Mhina, Mohamed Yussuf Nuh, Ali Salim Khamis na Abdalla Mussa Hija.

Kutangazwa kwa kamati hiyo ya pamoja ni hatua muhimu ya kuendeleza ufuatiliaji wa makubaliano yaliyofikiwa na CCM na ACT Wazalendo baada ya mazungumzo yaliyochukua miezi minane kuanzia Novemba mwaka jana - 2026, yaliyofikia tamati kwa kutolewa tamko la pamoja Julai 9 Julai, mwaka huu.

  • zanzibar
  • suk
  • mwinyi
  • amani
  • ccm
  • act

Soma Pia