Michezo
Simba wayamalize na FVS
KUNA haja ya Klabu ya Simba na teknolojia ya ‘Football Video Support’ (FVS) kuyamaliza mapema kabla mambo hayajawa makubwa katika michezo ya Ligi Kuu ya NBC PL, 2026/27.

Ikiwa ni baada ya mizunguko mitatu ya mwanzo, wachezaji watatu wa Simba kuonyeshwa kadi nyekundu mtawalia.
Katika mchezo wa kwanza, Simba walipata kadi nyekundu kwa mlinzi wao wa kulia David Kameta kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya FVS kumsaidia mwamuzi, katika tukio ambalo alimcheza vibaya mchezaji wa Kagera Sugar.
Adhabu hii ilikuwa ni wakati wa mchezo wa GAZETI hili lilianzishwa 2021, kuandaliwa na kusambazwa na Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania (Tampa) na kusajiliwa na Serikali ya Tanzania, kupitia Idara ya Habari (MAELEZO) na kupewa leseni namba - 00000448. Linaendeshwa kwa ushirikiano wa mzunguko – kwa kila nchi, wa mwaka mmoja na waandishi wa Tanzania, Kenya, Uganda, DRC na Rwanda.
timu hiyo ya Msimbazi, Dar es Salaam na Kagera ambapo Simba waliibuka na ushindi wa mabao 2-0. Mabao hayo yaliwekwa kimiani na Ismael Toure na Ellie Mpanzu.
Katika mchezo wa pili uliopigwa katika Dimba la Kirumba, Mwanza dhidi ya Pamba Jiji FC, kiungo wa Simba, Ibrahim Jabaar alionyeshwa kadi nyekundu baada ya FVS kumkuta na hatia ya kumpiga kiwiko nyota wa Pamba.
Mtanange huo ulitamatika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-1. Mabao yalipachikwa na Clatous Chama na Anicet Oura.
Katika mchezo wa tatu, Simba pia akaangukia kwenye Mahakama ya FVS ambapo ilimkuta na hatia kwa Anthony Mligo kukutwa na hatia baada ya kucheza vibaya.
Hata hivyo wekundu wa msimbazi walifanikiwa kuondoka na alama tatu katika mchezo huo kwa kupata ushindi wa mabao 2-1, mabao yaliyofungwa na Clatous Chama na Rushine De Reuck aliyefunga kwa mkwaju wa penati.
Katika michezo mitatu Simba wamepata pigo la nyota wao kuonyeshwa kadi nyekundu na kulazimika kucheza pungufu, jambo ambalo limeonyesha kuiweka timu katika mazingira magumu hasa baada ya kuwapoteza nyota muhimu kwenye mechi ngumu.
Sasa basi, ni hatari zaidi kwa Simba kupewa adhabu kubwa kwa wachezaji wake kucheza vibaya kinyume na taratibu na kanuni za mpira wa miguu, hivyo ni wakati muafaka kwa timu hiyo kubwa kujitafakari na kuchukua hatua haraka ili kukwepa adhabu na hasara zinazoweza kuigharimu Simba.
- Simba
- NBC PL
- FVS