Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Michezo

Steven Gerrard atia neno Liverpool

NYOTA wa zamani katika klabu ya Liverpool, Steven Gerrard amesema klabu hiyo imeanza msimu kiulaini mno hali inayotishia kutokuwa na makali ya kuwania taji la Ligi Kuu ya England msimu huu.

Jumatatu, 31 Agosti 2026 · 06:00Dakika 1 kusomaToleo 180, uk. 37
Mchezaji wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrard
Mchezaji wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrard — Picha kutoka mtandaoni

Kufuatia kusuasua kwa safari yake ya ushindi, amemtaka Kocha Andoni Iraola kuongeza wachezaji wakatili katika maeneo muhimu.

Kauli ya Gerrard imekuja mara baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Nottingham Forest Jumamosi iliyopita katika Dimba la Anfield.

“Nadhani Liverpool hii ni timu laini mno. Hawana mtu wa kuharibu mipango ya timu pinzani, atakayeshinda mapambano na mzuri uwanjani...”

“Hivyo wanapaswa kupata mtu katili ndani ya uwanja ambaye atailinda timu na kuifanya kuwa salama kutekeleza mpango kazi wa kupata matokeo kwenye michezo yao,” alisema Gerrard akiambia TNT Sports na kuongeza kuwa.

“Kuna muda unashinda mchezo kwa njia tofauti, kikosi kina wachezaji wazuri sana kimbinu na wenye vipaji lakini kinakosa mtu wa kazi, nadhani kocha anajukumu la kumpata huyo mtu aje kuisaidia timu.

“Vinginevyo kama hawatapata mtu wa kuja kuifanyia timu kazi ngumu katikati ya uwanja sio rahisi kushinda taji, mwishoni mwa msimu hawatashinda chochote zaidi ya kuwa watazamaji.

Liverpool wamecheza michezo miwili sawa na dakika 180 wakitoka sare michezo yote, dhidi ya Newcastle 2-2 na dhidi ya Nottingham Forest 2-2. Pointi mbili, nafasi ya 11 kwenye msimamo wa EPL.

  • Liverpool
  • EPL
  • Steven Gerrard

Soma Pia