Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Burudani

Sugu awataka wasanii kuwekeza

MWANAMUZIKI mkongwe wa Hip Hop nchini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu, amewataka wasanii kutumia umaarufu wao kuanzisha na kukuza biashara badala kutegemea sanaa pekee.

Jumatatu, 10 Agosti 2026 · 17:15Dakika 1 kusomaToleo 177, uk. 40

Sugu ambaye pia ni mwanasiasa na mfanyabiashara, ametoa rai hiyo juzi jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa duka lake la kubadilisha fedha za kigeni aliyoipa jina la Desderia Bureau de Change.

“Wasanii, wanamichezo na watu wote maarufu wanapaswa kutambua kuwa majina yao ni mtaji…”

“Wakiyatumia vizuri wanaweza kuanzisha biashara mbalimbali na kujitengenezea fursa za maendeleo badala ya kutegemea umaarufu pekee,” amesema Sugu.

Amesema kuanzishwa kwa Desderia Bureau de Change ni sehemu ya juhudi zake za kuwekeza katika sekta rasmi ya biashara na kuhamasisha watu wengine hasa wenye majina makubwa kutumia fursa hiyo.

  • Sugu
  • Wasanii
  • Biashara

Soma Pia