Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Hoja Yangu

Tatizo la taka mijini ni zaidi ya madampo

KILA siku tunapozungumzia usafi wa Dar es Salaam, macho yetu mara nyingi huangalia taka zilizo pembeni mwa barabara, kwenye mitaro au maeneo ya wazi.

Jumatatu, 28 Septemba 2026 · 06:00Dakika 1 kusomaToleo 184, uk. 27

Lakini ziara ya Makamu wa Rais wa Tanzania, Deogratias Ndejembi, katika Dampo la Pugu hivi karibuni imerudisha swali muhimu zaidi; tatizo la taka ni la dampo au ni la namna tunavyopanga na kuendesha miji yetu?

Septemba 18, Makamu wa Rais Ndejembi aliagiza Dampo la Pugu kuboreshwa, maeneo yanayozunguka dampo kupuliziwa dawa na mamlaka kuhakiki takwimu zinazotofautiana kuhusu kiasi cha taka kinachokusanywa kila siku.

Alisisitiza kuwa bila taarifa na takwimu sahihi, ni vigumu kutatua tatizo hilo.

Hapo ndipo mjadala mpana unapopatikana, na ndipo ilipo Hoja Yangu.

Dar es Salaam ilikadiriwa kuzalisha takribani tani 4,600 za taka kwa siku, huku chini ya asilimia 40 zikikusanywa na kupelekwa katika maeneo rasmi ya utupaji. Dampo la Pugu lenye ukubwa wa takribani hekta 66 limekuwa sehemu kuu ya mfumo huo.

Takwimu hizi zinatufundisha jambo moja: Pugu si tatizo la Pugu pekee. Ni picha ya mfumo mzima wa usimamizi wa taka jijini Dar es Salaam.

Kama taka zinazalishwa kwa kasi kubwa kuliko uwezo wa kuzikusanya, kusafirisha, kuchakata na kuzitupa kwa usalama, hata tukiboresha dampo leo, kesho tatizo linaweza kurudi. Hii ndiyo Hoja Yangu.

Ndiyo maana kauli za hivi karibuni kuhusu kugeuza taka kuwa fursa ya kiuchumi zina umuhimu. Mkoa wa Dar es Salaam umeanza kuangalia uwezekano wa kushirikisha sekta binafsi katika kuchakata taka na kuzalisha bidhaa kama mbolea na gesi.

Umebakiwa na makala 2 za bure mwezi huu. Jiunge ili kusoma bila kikomo.

  • Taka
  • Miji
  • Mazingira
  • Usafi

Soma Pia