Biashara
Tiseza: Dola bilioni 15.32 za uwekezaji zaingia ndani ya mwaka mmoja
Mamlaka imesajili miradi 1,148 inayotarajiwa kuzalisha ajira 344,031, lakini changamoto ni kugeuza ahadi hizo kuwa viwanda, ajira halisi na ukuaji wa uchumi.

MAMLAKA ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) imesajili miradi 1,148 yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 15.32 katika kipindi cha Julai 2025 hadi Septemba 2026, ikitarajiwa kuzalisha ajira zaidi ya 344,031.
Takwimu hizo zinaashiria fursa kubwa kwa uchumi wa Tanzania, hasa katika kupanua uzalishaji wa viwandani, kuongeza ajira na kuvutia mitaji ya ndani na nje. Hata hivyo, mafanikio ya uwekezaji hayawezi kupimwa kwa thamani ya miradi iliyosajiliwa pekee, bali kwa kiasi cha mitaji kilichoingia nchini, miradi iliyoanza uzalishaji na ajira zilizozalishwa.
Katika mkutano na wahariri ulioandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, taarifa ya mafanikio ya TISEZA, iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa taassisi hiyo, Gilead Teri, iliweka wazi hatua zilizopigwa pamoja na changamoto zinazohitaji kushughulikiwa ili uwekezaji uwe na mchango unaopimika katika uchumi.
Mkutano huo uliratibiws na Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR) chini ya mkakati wa ofisi hiyo wa kuyakutanisha mashirika ya umme na waandishi wa habari ili kuyawezesha kueleza mambo wanayoyafanya.
Kikomo cha bure kimefikia
Umesoma makala 3 za bure mwezi huu
Jiunge ili kuendelea kusoma bila kikomo, au ingia kama tayari una uanachama.
Mwezi
TSh 8,000
kwa mwezi
Mwaka
TSh 80,000
kwa mwaka
Au fungua akaunti ya bure ili hesabu yako ifuatane nawe kwenye vifaa vyote.
Lipa kwa M-Pesa · Mixx by Yas · Airtel Money · HaloPesa