Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Uhusiano

Vijana waepuke kuiga kila kitu, wafikiri zaidi

Mara nyingi, hasa nyakati hizo, vijana wamekuwa wepesi wa kuiga kila wanachoona wenzao wanafanya bila kufikiria vyema, sasa hapa mwanasafu ya uhusiano anajadili jambo hili.

Jumatatu, 28 Septemba 2026 · 06:00Dakika 1 kusomaToleo 184, uk. 40
Kuiga kuvuta shisha na ulvi mwingine kumewakumbaz aidi vijana.
Kuiga kuvuta shisha na ulvi mwingine kumewakumbaz aidi vijana. — Picha kutoka Maktaba

NAKUSALIMU msomaji wangu wa Safu ya Uhusiano na karibu uweze kupata elimu kuhusu masuala mbalimbali.

Wiki iliyopita nilizungumza namna uthibiti wa kinywa utakavyoweza kukusaidia kujiepusha na mambo yasiyofaa na wiki hii nitazungumza umuhimu wa vijana kuepuka kujiunga na makundi mabaya.

Vijana ni nguvu ya taifa, ni kesho ya nchi yetu. Lakini leo hii, changamoto kubwa inayowakabili ni kujitumbukiza kwenye makundi mabaya kwa kutaka kujiona wa kisasa.

Wengi wa vijana hurubuniwa na kujiingiza kwenye makundi ya ulevi, dawa ya kulevya, wizi na ujambazi, anasa na uasherati mitandaoni, au makundi ya vurugu shuleni.

Vijana huingia humo kwa kurubunika na maneno matamu ya marafiki kwa kuambiwa ‘jaribu tu mara moja’, ‘kila mtu anafanya’ au maneno kama ‘utakuwa hodari ukijiunga nasi.’ Kwa mfano leo hii kijana ambaye bado yuko shule akirubuniwa na wenzake na kuingizwa kwenye kundi la wameza dawa za kulevya kisha akaona matunda yake (ya haraka haraka) na kuamua kuacha shule na mwisho wake huwa mbaya.

Vijana watambue kuwa madhara ya makundi hayo ni makubwa kwani mwisho wake huwa mbaya.

Vijana wanatakiwa kujikita kwenye masuala muhimu lakini pia kuchagua marafiki bora ambao watashauriana mambo ya msingi kuliko kujiingiza kwenye makundi mabaya.

Lakini pia watambue thamani yao na kamwe wasikubali kutumika vibaya kwani kila mmoja ana alama yake njema. Waseme hapana kwa ujasiri pale wanaporibuniwa na pia kuwa karibu na Mungu na familia.

Tukutane wiki ijayo.

  • vijana
  • uhusiano
  • mkumbo

Soma Pia