Rukia maudhui makuu
Pambazuko
Ukweli Hauna Kutu

Habari Kuu

Watatu wapandishwa kizimbani tuhuma za ugaidi

Kesi za ugaidi bado zinaendelea na leo watu wengine wamefikishwa mbele ya mahakama kwa tuhuma hizo nzito. Ukiacha watu hawa, bado kuna kesi za uzito huo zinazoendelea kwenye korti za Tanzania.

Jumatano, 18 Novemba 2026 · 16:59Dakika 1 kusoma
Colleta
Colleta — Picha kutoka Maktaba ya Pambazuko

WATU watatu wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, na kuunganishwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Mkoa wa Kigoma, Colletha Ntidyicha, katika kesi ya ugaidi.

Colletha, alipandishwa kizimbani katika mahakama hiyo ambapo alisomewa shtaka la ugaidi Novemba 3, 2026, siku moja baada ya amri ya Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam.

Novemba 2, 2026 - Mahakama Kuu, ililiamuru Jeshi la Polisi limfikishe mahakamani au limwachie kwa dhamana, Colletha baada ya maombi aliyoyafungua kupitia mawakili wake, akipinga kushikiliwa kizuizini na Jeshi la Polisi kwa muda mrefu kuanzia Oktoba 14, 2026 bila kufikishwa mahakamani au kupewa dhamana kinyume na sheria.

Hata hivyo, alifutiwa kesi hiyo badala yake Jamhuri ikabadilisha hati ya mashtaka kwa kumuunganisha na watu wengine watatu waliofikishwa mahakamani hapo, kisha wakasomewa mashtaka mawili.

Waliounganishwa na Colletha ni Doris Msingwa (32) mkazi wa Arusha, Alex Kyai (42), dereva na fundi nguo, Juma Kijazi (29), wote wawili wakazi wa Mtoni Kwa Aziz Ally, Dar es Salaam.

Chanzo: Pambazuko Digital

Umebakiwa na makala 2 za bure mwezi huu. Jiunge ili kusoma bila kikomo.

  • Ugaidi
  • Mahakama
  • Kisutu
  • Kesi

Soma Pia

Watatu wapandishwa kizimbani tuhuma za ugaidi | Pambazuko